Kwa mujibu wa jukwaa maaarufu la watafiti wa masuala ya ubora wa simu janja Duniani, @dxomark wametoa orodha ya simu janja 5 zenye ubora katika vioo ‘Display’ kwa mwaka 2021.
Kwenye Orodha hiyo iliyokuwa inashikiliwa kwa muda mrefu na Toleo la Galaxy S21 Ultra kutoka Samsung na simu ya Huawei P50 Pro kutoka katika Kampuni ya Uchina ya Huawei, Kwasasa inashikiliwa na Matoleo mapya ya iPhone 13 Series kutoka Katika Kampuni ya Apple, Ambapo iPhone13 Pro Max na iPhone13, Yameshika Namba moja na Mbili.
Je, Kuna Kampuni ya simu ambayo inaweza kupindua matokeo kwa mwaka huu…? Unaweza kuacha maoni yako hapo chini;