Dj Adams na binti yake Nadine ambaye hajulikani aliko

Mtangazaji mkongwe nchini Rwanda ambaye pia ni Dj Adam Aboubakar almaarufu Dj Adams, anadai mtoto wake wa kike hajulikani aliko tangu siku tatu zilizopita.

Uwimpaye Nadine ‘Nice’ alimuaga baba yake mnamo Disemba 18, 2020 ambapo alimpigia na kumuambia hatamuona tena na kisha kukata simu kwa sababu anazozijua yeye tu.

Adams amesema Nadine alimpigia hata mama yake na kumfikishia ujumbe huo na kisha kutaka simu, na wote walipompigia kutaka kujua kilichomsibu simu zao hazikupokelewa mpaka sasa.

Nadine alikuwa anaishi na baba yake maeneo ya Muhima Mjini Kigali, na tangu kuondoka kwake baba yake amekosa furaha kutokana na kutojua mtoto wake alipo na kilichomfanya aikimbie kaya.

Dj Adams amesema katika juhudi za kumtafuta mtoto wake huyo ambaye ndiye wa kwanza kuzaliwa, aliwatoa taarifa RIB (Idara ya Taifa ya Upelelezi) lakini jitihada zao kuhakikisha upatikanaji wake hazijazaa matunda yoyote.

Adams ambaye ana umri wa miaka 44, ana watoto wawili ambao ni pamoja na Nadine mwenye umri wa miaka 20 huku mtoto wa kiume Adam Aboubakar Junior akiwa ana miaka 6.

Watoto hao wawili  wanaishi na mama zao tofauti ambao pamoja na kwamba walizaaa na Adams lakini hawajawahi kuishi naye chini ya dari moja.

Adams alianza shughuli za DJ mwaka 1993 Nairobi nchini Kenya ambako ndiko alikozaliwa.

Alikuja kujizolea umaarufu mkubwa nchini Rwanda hata kupitia kazi za utangazaji hasa kutokana na anavyowaponda wasanii wa Rwanda akisema hawana dira.

Alitangazia redio lukuki ikiwemo City Radio, Radio One, Hot FM na Radio 10 ambayo ndiyo mwajiri wake siku hizi.

Imeandikwa na Janvier Popote

LEAVE A REPLY