Rais Kagame akisalimiana na Benjamin Mkapa mwaka 2016.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ametoa agizo kwamba bendera ya Rwanda popote ilipo na ile ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki zipepee nusu mlingoti kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Tanzania, William Benjamin Mkapa.

Benjamin Mkapa alikuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo bado hayajawekwa bayana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyoko Jijini Dar es Salaam.

Aliaga dunia usiku wa kuamkia jana kwa mujibu wa tangazo la rambirambi lililotolewa na Rais John Magufuli. 

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameagiza bendera husika zipepee nusu mlingoti kwa muda wa siku tatu kuanzia Jumatatu, Julai 27 kwa ajili ya kuomboleza kifo cha rais huyo wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliingia mamlakani mwaka 1995 na kuhudumu kwa muda wa miaka 10.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu ikimnukuu Rais Kagame inaonesha ametoa pole zake kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia ya marehemu na Serikali ya Tanzania katika kipindi hiki kigumu.

LEAVE A REPLY