Mawakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi , maarufu Bobi Wine wamewasilisha ushahidi zaidi katika mahakama ya juu zaidi nchini humo dhidi ya matokeo ya uchaguzi uliomrejesha tena madarakani Rais yoweri Museveni.
Jopo la majaji likiongozwa na Jaji mkuu Alfonce Owiny Doro, linasikiliza ombi hilo katika Mahakama ya juu zaidi hivi sasa.
Hii inakuja baada ya mawakili wa upande wa Bobi Wine kuiomba mahakama waongeze ushahidi zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi Januari.
Rais Museveni alipata ushindi wa asilimia 58.08 huku Robert Chagulanyi akipata asilimia zaidi ya 35, matokeo yanayopingwa vikali na Bw Wine.
Upande wa mawakili wa Rais Museveni umeshapokea nakala ya mashtaka na siku ya Alhamisi wiki hii wanatarajia kufika katika mahakama ya juu kupanga siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, katika kipindi cha siku 45 kulingana sheria ya uchaguzi nchini humo.
Chanzo: BBC