Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya viriusi vya Corona. AFP / LUIS TATO

Wauguzi nchini Kenya wanatishia kugoma wiki ijayo, iwapo hawatalipwa marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi kipindi hiki ambacho nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Tishio hilo limekuja wakati watu wengine 690 wakipatikana na virusi hivyo kwa muda wa  24 zilizopita, na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa nchini humo kufikia 22,053.

Kenya ina visa 22,053 vya maambukizi, huku ikirekodi vifo 369 kutokana na virusi vya ugonjwa huo hatari.

Wagonjwa 8,477 wamepona ugonjwa wa Covid-19.

Kamati ya dharura ya shirika la Afya duniani, WHO, inayofanya tathmini mpya kuhusu janga hilo, imesema janga hilo linatarajiwa kuwa la muda mrefu na kutaja umuhimu wa kudumisha juhudi za kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa za kukabiliana na virusi hivyo.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, shirika hilo la WHO limesema linaendelea kukadiria kiwango cha hatari cha kimataifa cha Covid-19 kuwa juu sana.

Chanzo: RFI

LEAVE A REPLY