Bushiri and his wife

Mchungaji Bushiri, ambaye alisema kuwa anataka kusafisha jina lake, amerejea katika nchi yake, Malawi, akiwa na mke wake Mary.

Mapema mwezi huu, alikuwa ameachiwa jela kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa utapeli na utakatishaji fedha.

Alisema kulikuwa na majaribio kadhaa ya kutishia maisha yake na mamlaka ya Afrika Kusini haikutoa ulinzi wowote kwake.

Bwana Bushiri ameelezea suala lake la kukwepa dhamana ni njia ya busara ya kulinda maisha yake, akiongea katika mitandao ya kijamii.

Swali likiwa ni namna gani mchungaji huyo ameweza kutoroka Afrika Kusini na kurudi kwao.

Kuna madai kuwa bwana Bushiri alitoroka na ndege ya rais wa Malawi akiwa na rais Lazarus Chakwera-jambo ambalo ofisi ya rais wa Malawi inakanusha kuhusika.

Maswali mengine yakihoji kama mataifa hayo mawili yatashirikiana kumkamata na kumrejesha Afrika Kusini asikilize kesi yake.

Waziri wa sheria wa Afrika Kusini Ronald Lamola alisema serikali haitasita kufuatilia suala hilo.

Lakini waziri wa mambo ya nje nchini Malawi, Eisenhower Mkaka atahusishwa katika suala hilo.

Amemwambia mwandishi wa BBC’ Nomsa Maseko kuwa ni jukumu la serikali kulinda raia wa Malawi lakini aliongeza kuwa rais Chakwera ni mtetezi wa sheria na mianya yote ya kidiplomasia itabaki wazi.

Mchungaji Bushiri ni nani?

Ni mchungaji milionea ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa miongoni mwa wachungaj tajiri zaidi barani Afrika.

Alitajwa kuwa na matukio tata; alisema aliwaponya watu na virusi vya ukimwi , alifanya vipofu waone, alionekana akitembea kwenye hewa.

Amekulia katika kijiji cha Mzuzu, Malawi na kuhamia Pretoria Afrika Kusini ambako ndio kulikuwa na kanisa lake – ‘the Enlightened Christian Gathering’.

Alipata umaarufu kwa kujaza umati wa watu kwenye mahubiri yake kwenye viwanja vya mpira.

Mchungaji huyu anashutumiwa nini?

Bwana Bushiri anashutumiwa kufanya utakatishaji fedha, utapeli na kufanya matukio ya uhalifu akiwa yeye na mkewe na watu wengine watatu.

Kesi yake inajumuisha mamilioni ya dola.

Kesi ilikuwa imefikia wapi?

Mchungaji alifikishwa mahakamani Oktoba 21, kusikiliza kesi zake na kupewa dhamana mwezi Novemba.

Kesi yake ilipangwa kuanza kusikilzwa mwezi Mei.

Chanzo: Bongo5

LEAVE A REPLY