Sgt Meja Robert Kabera

Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limesema limeanza upelelezi juu ya madai ya ubakaji yanayomkabili afisa wake Sergeant Meja Robert Kabera.

Taarifa ya RDF kwa umma inasema aliyebakwa ni mtoto mwenye umri wa miaka 15 ambaye ana uhusiano wa kifamilia na Sergeant Meja Kabera.

Aidha, tangazo linaeleza kitendo hicho cha kinyama kilitekelezwa mnamo Novemba 21, 2020 katika Tarafa ya Ndera, Wilayani Gasabo, Mjini Kigali.

Sergeant Meja Robert ni nguzo muhimu kwenye bendi la Army Jazz Band, bendi ya RDF inayojikita kuhusu nyimbo za kuyasifia majeshi ya Rwanda na ushujaa wake.

Sergeant Meja Robert Kabera amejizolea umaarufu mkubwa kwenye ulingo wa muziki nchini Rwanda kupitia nyimbo zake za kidunia na zile za injili kama Impanda (Parapanda)

Anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka hadi 25 kwa mujibu wa ibara namba 133 ya sheria ya makosa ya jinai yam waka 2018.

Na kama aliyebakwa ana miaka chini ya 15, adhabu huwa ni kifungo cha maisha jela.

Mshukiwa hajulikani aliko tangu kufanyika ubakaji, lakini Jeshi la Rwanda limeahidi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake.

Imeandikwa na Janvier Popote

LEAVE A REPLY