Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania Oktoba mwaka huu, baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kuzindua rasmi kampeni za kuwanadi wagombea wao wa viti vya ubunge, uwakilishi, udiwani na Rais.
Kwa upande wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wao wanazindua kampeni kitaifa, kanda ya Pwani, siku ya leo.
Chama cha mapinduzi (CCM) kinatarajia kuzindua kampeni zake kesho, katika mjii mkuu wa nchi hiyo Dodoma.
Kwa upande wa chama cha ACT Wazalendo wao bado hawana uhakika wa kampeni zao zitaanza lini ama kufanyika wapi.
Kwa upande wa vyama vingine vya siasa, bado hawajatoa taarifa rasmi za utaratibu wa kampeni zao.
Uchaguzi wa Tanzania unatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Chanzo: BBC
Asante sana kwa habari unazotuletea huwa zinavutia na kuelimisha zaidi. Hongera sana Popote.